fbpx
31 Jan
08:00

Kujiandaa na Mitihani

JINSI YA KUJIANDAA NA MITIHANI

Kila mtu anataka kufaulu vizuri na kuwa na marks nyingi katika mitihani na majaribio. Moja ya sababu kwanini tunaenda shule ni kusoma na kuelewa vizuri hatimaye kupata matokea mazuri katika mitihani yetu.

Mara nyingine hutokea mwanafunzi anakuwa amesoma sana lakini bado asifanye vizuri katika masomo. Hii ni kwa sababu huwa hajajiandaa vya kutosha kufanya mitihani.

Mbinu za kujiandaa vizuri na mitihani

  • Panga ratiba yako ya kujisomea kila siku na uhakikishaeunaifuta vyema.
  • Tumia masaa machache kila siku kurudia masomo uliyofundishwa kwa siku hiyo badala ya kusoma masomo yote kwa pamoja.
  • Fanya majaribio mengi. Kwa mfano ukiwa na Application ya SmartSchool ExamMaster unaweza ukafanya majaribio mengi unavyotaka na ukaangalia maendeleo yako kwa urahisi. Mwanafunzi anaweza kujua ni eneo gani linahitaji kuwekewa mkazo katika kujifunza na kujiandaa vizuri zaidi.
  • Tumia muda mwingi kuelewa unachotaka kujua badala ya kukariri vitabu. Kuelewa vizuri hukusaidia kukumbuka kiurahisi na kujibu mitihani yako vizuri zaidi.
  • Angalia muda unaotumia kujibu maswali.kwa mfano somo kama Hesabu hutumia muda mwingi kusoma. Lakini mazoezi mengi huongeza kasi ya kujibu maswali na kukufanya ufanye vizuri katika mitihani yako.
  • Jipatie muda wa kupumzika. Ubongo wa binadamu huwa unachoka pia. Hivyo ni muhimu kupata mapumziko ya muda mfupi kila baada ya muda kuruhusu akili/unongo kupumzia.hii itakusaidia kusoma kwa muda mrefu bila kuchoka au kuboreka.
  • Maliza kwanza masomo magumu au anza na masomo magumu. Hii itakuondolea wasiwasi wa mambo magumu ambayo bado hujasoma pindi mitihani inapokaribia
  • Tumia vifaa sahihi na vitabu vya uhakika kusoma ili kuweza kuelewa vizuri kwa usahihi na uhakika.

 

Tunakutakia mafanikio katika mitihani yako, uwe na matokeo mazuri yakushangaza.

Tag: ElimuNiMali ,SmartSchool