fbpx
03 Feb
08:00

Jinsi Ya Mwanafunzi Kufurahia Muda Wake Akiwa Shuleni

Wanafunzi wa siku hizi hujishughulisha na mambo mengi kiasi cha kukosa muda wa kusoma vizuri. Muda mwingi utasikia wakisema “lakini dada sina muda wa kufanya kazi za shule nyumbani au kujiandaa na mitihani”, Hawa wanafunzi mara nyingi kuanzia umri wa miaka 13-19 hujiingiza katika shughuli nyingi ambazo hupoteza muda wao.

Kwa mfano;

  • Hutumia muda mwingi sana kwenye mitandao ya kijamii kama (Facebook, Instagram, Snapchat n.k)
  • Kutoka kwenda sehemu za kustarehe na marafiki zao kuliko inavyoshauriwa.
  • Kucheza michezo ya kwenye sinema
  • Kuchat Whatsapp masaa mengi mno
  • Kuweka akili zao kwenye shughuli za michezo na starehe kuliko kwenye masomo.

Moja ya sababu zinazofanya wanafunzi kujisahau na kutumia muda mwingi kufanya mambo mengine ni kwamba hawafurahii kusoma. Kusoma vitabu vikubwa kunachosha. Hivyo inashauriwa kujifunza kupitia vifaa stahiki vitakavyowavutia kujifunza bila kuchoka wala kuboreka. Moja ya vifaa hivyo ni SmartSchool. Huu ni mfumo wa kujifunza kupitia sinema zilizotengenezwa kwa ubora wa hali ya juu. Zimesheheni masomo yote mwanafunzi wa kitanzania anahitaji. Imepitishwa na baraza la elimu kutumika mashuleni. Kwa kutumia hii mwanafunzi anaweza kijifunza na kufanya majaribio mengi ili kuangalia kama ameelewa vizuri.

 

Pia kuna mambo mengine mwanafunzi anaweza kufanya ili kutumia muda wake vizuri;

  1. Tengeneza ratiba. Hapa mwanafunzi anaweza kutenga muda kwa kila shughuli. Kwa mfano saa moja baada ya masomo –Facebook. Dakika 30 kabla ya kulala – Whatsapp. Masaa mawili baada ya shule – kujisomea. Hii itamsaidia mwanafunzi kujenga nidhamu katika maisha.

 

  1. Epuka kughairi. Wanafunzi hupendelea kuacha kufanya shughuli zao mpaka dakika za mwishoni. Hii hutokana na kukosa shauku ya kusoma au mambo kuwa magumu.

 

  1. Weka kipaumbele sawa. Ni muhimu mwanafunzi kupangilia kazi zake kulingana na umuhimu wake. kushinda kwenye michezo na kufaulu mitihani ya mwisho vyote vinaumuhimu sawa. Hivo kutoa kipaumbele kwenye kitu kimoja husabaisha matokeo yasiyoridhisha kwenye kitu kingine.

 

  1. Mpangilio, ni vizuri mwanafunzi kuweka mpangilio kati ya masomo na michezo. Ni muhimu kwa mwanafunzi kuwa na mpangilio na kuweka malengo kwa siku na kwa mwaka pia. Kwa mfano masaa mawili yakujisomea kila siku, kufanya majaribio ya mitihani iliyopita kila mwezi, kujiandaa na darasa la muziki wiki tatu.

 

Hivyo basi ni muhimu kwa kila mwanafunzi kupangilia muda wake vizuri. Sio tu kwa kufaulu mitihani vizuri bali kuweza kupata nafasi yakufurahia michezo na shughuli nyingine kwa furaha bila hofu.

Tag: ElimuNiMali ,SmartSchool