fbpx
26 Jan
11:55

Kingereza Kama Lugha ya Kimataifa

Kingereza – Lugha ya Kimataifa

Umuhimu wa kusoma, kuandika na kuongea kiingereza kwa ufasaha

Watu wote tumetoka maeneo tofauti tofauti na kuongea lugha mama tofauti tofauti.  Kuongea lugha zetu za asili inaweza kuwa ni njia bora sana ya kuwasiliana. Hata hivyo katika ulimwengu wa sasa ni muhimu sana kujua kusoma, kuandika na kuongea kiingereza kwa ufasaha. Kiingereza kinazungumzwa na watu takriban million 375 duniani na nchi zaidi ya 50 hutumia kiingereza kama lugha yao rasmi ya awali.

Kwa wale watu ambao hutumia kiingereza kama lugha yao ya pili wanaelewa jinsi ilivyo kazi kutamka maneno magumu. Au kutofautisha maneno yanayotamkwa sawa lakini yakiwa na maana tofauti. Kwa mfano right na write, lie na lay, there na their. Kuondoa hii changamoto ni muhimu watoto wetu wakajifunza kiingereza katika umri mdogo.

Watoto hujifunza lugha mpya kwa haraka kuliko watu wazima. Kama wazazi inabidi tuhakikishe watoto wanajifunza kuandika kila tarakimu mara tu wakianza kushika kalamu au rangi za kuchora. Kuweka msingi wa kitu chochote huanza katika umri mdogo. Na nimuhimu kuwakazania watoto kujua kusoma, kuandika na kuongea kiingereza pasipo kutumia nguvu yoyote. Hii itawasaidia kufaulu vizuri katika mitihani na kuwasiliana kwa lugha ya kiingereza bila kupata ugumu wowote.

Faida za kujua kusoma, kuandika na kuongea kiingereza

  • Mwanafunzi anaweza kuelewa kitu vizuri na kwa urahisi zaidi
  • Hupanua mawazo na kukuza lugha yake kila siku
  • Kwa kusoma unapunguza makosa ya kimatamshi
  • Itamsaidia mtoto wako kuweza kuishi mahali popote duniani
  • Lugha hii itamuongezea ujuzi wakujieleza na kufanya mawasiliano na watu.
  • Itamsaidia katika kufanya vizuri ka tika masoma yake, kwa kuwa atakuwa anaelewa vizuri na kwa haraka
  • Itamsaidia kujiamini zaidi

 

Uwezo wa mtoto kusoma, kuandika na kuongea kiingereza humpa nguvu ya kuungana na ulimwengu wa sasa bila wasiwasi. Ili mtoto apate huo uwezo inabidi kumjengea misingi imara akiwa bado mtoto ili kuendelea kumuimarisha hata kwa hapo baadae.

Tag: ElimuNiMali ,SmartSchool