Mara tu calendar inapoanza mwezi wa kumi, kila mtu anawaza likizo na sikukuu zinazofungamana nazo. Hali ya hewa huwa ni nzuri sehemu nyingi hivyo watu huanza kufikiri jinsi watakavyo tumia likizo zao, sikukuu za Eid, Christmass, Mwakampya na nyenginezo kufurahi na ndugu, jamaa na marafiki wa karibu.
Pamoja na sikukuu zote hizi na muda wa kupumzika, ukiwa mwanafunzi bado inakulazimu kwenda shule, kusoma vitabu, kuingia library kujisomea, kufanya majaribio ya kisanyansi na mambo mengine mengi ya kielimu yanayoweza kukufanya usifurahie wakati wa likizo na sikukuu kwa raha. Hivyo basi ni vizuri sana kutoruhusu msimu huu wa sikukuu kukuharibia mwelekeo wako wa elimu katika kutimiza ndoto zako.
Ondoa vipingamizi.
Vipingamizi au vizuizi huwa vipo kila wakati, lakini kwa msimu huu wa sikukuu huongezeka sana kutokana na muda mwingi unaohitajika kuwa na familia, marafiki na ndugu wa karibu hivyo kutengeneza muda kwa ajili ya masomo huwa ni ngumu sana kipindi hiki.
Na hapa ndio tunasema nidhamu katika elimu ni kitu muhimu sana kwa mwanafunzi kuliko vyote. Inabidi uweze kufurahi na kusherekea muda wako na familia lakini ni muhimu pia kuweka usawa kati ya masomo na muda wa kupumzika.
Dondoo za jinsi ya kusoma wakati wa likizo
Hapa tumekuwekea vitu vichache vinavyoweza kukusaidia kufurahia likizo yako bila kupoteza hamu ya kusoma wakati wa likizo.