fbpx
08 Aug
01:20

MKOMBOZI WA WANAFUNZI APATIKANA – SIKUKUU YA NANENANE

Leo ni tarehe 8 mwezi wa 8 mwaka 2018. Tarehe na mwezi kama huu kila mwaka Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Watanzania wote kwa ujumla husherehekea sikukuu ya wakulima, maarufu kama  NANENANE. Wakulima wote wakubwa na wadogo huitumia siku hii kuonesha kazi zao ikiwa ni namna moja  ya kujifunza kutoka kwa wakulima wenzao njia bora za uzalishaji na kilimo bora na pia kuuza bidhaa zao.

Kwa kusherehekea siku hii SmartSchool Tanzania inakutangazia sasa mkombozi wa wanafunzi amepatikana. SmartSchool Tanzania imeandaa programu maalumu ya kumwezesha mwanafunzi kujisomea ili hatimaye tuweze kuwa na watoto wa wakulima waliosoma na vilevile kutengeneza tabaka la wakulima wenye elimu bila kuangalia ni wakulima wakubwa au wadogo, ili kuzidisha kasi ya uzalishaji na uboreshaji wa Sekta ya kilimo kwa ujumla. Uboreshaji wa sekta  ya kilimo utaleta mabadiliko chanya katika sekta yenyewe ya kilimo na sekta nyingine kama vile sekta ya viwanda na biashara kwa ujumla.

SmartSchool Tanzania ni mfumo wa kielektroniki umwezeshao mwanafunzi kujifunza kwa njia ya kidijitali kwa kutumia Kompyuta kwa njia tatu toafuti, njia ya kwanza ni njia ya kujifunza kwa kutumia video zilizotengenezwa kwa mfumo wa 3D yaani SmartSchool Tutor, njia ya pili ni kujifunza kwa mfumo wa maswali na majibu yaani SmartSchool Exam Master na njia ya tatu ni kujifuza kwa mfumo wa kufanya utafiti mtandaoni ya yale mwanafunzi aliyojisomea maarufu kama (research friendly platform) SmartSchool studio.

Vitini, michoro pamoja na maelezo yote yamehifadhiwa katika DVD, Flash pia sasa inapatikana kwa matumizi ya Tablet za Android. Wazazi na wanajamii kwa ujumla hawana budi kuwanunulia watoto wao program hizi ili kuongeza ufanisi katika masomo yao kwani programu ya Smartschool humwezesha mwanafunzi kukumbuka kwa urahisi aliyojifunza. Kwa maelezo zaidi tembelea kurasa zetu za mitandao ya kijamii za Facebook, Instagram na Twitter @Smartschool Tanzania au tovuti yetu ya www.smartschool.co.tz

Tag: Digital Learning ,e learning ,ElimuNiMali ,SmartSchool